KITUO CHA MAFUNZO CHA SILVERLANDS TANZANIA LIMITED (T-PEC) Follow
KITUO CHA MAFUNZO CHA SILVERLANDS TANZANIA LIMITED (T-PEC)
Chuo cha mafunzo kilianzishwa mwaka 2016. lengo ni kuwafikia wafugaji wadogowadogo, mashirika yasiyo ya kiserikali, Idara za serikali na kutoa mafunzo ya kuku kwa kina na kwa muda mfupi.
Chuo chetu kimekaa katika mazingira tulivu na mazuri, ili kuwawezesha watu wanaokuja kupata mafunzo kujifunza na kutengeneza urafiki. Tunajivunia kuwa sehemu ya mradi wa APMI, kufanya kazi na shirika la kuku ulimwenguni ili kuleta mabadiliko. Hadi sasa zaidi ya watu 2000 wamepita katika chuo chetu na wanatupatia mrejesho ulio bora kuhusiana na kozi zetu. Tunaendelea kutoa mafunzo haya kila mwaka, na hata kuongeza vituo vingine kulingana na uhitaji.
KUPITIA CHUO CHA MAFUNZO CHA SILVERLANDS UTAJIFUNZA KOZI ZIFUATAZO.
1.Ufugaji bora wa kuku wa Nyama (Broiler Course)
2.Ufugaji bora wa kuku wa Mayai (Layer Course)
3.Namna bora ya ufugaji na uzalishaji wa kuku kwa ujumla (Poultry Production)
Tunatoa mafunzo ya ufugaji kwa watu wote wanaoitaji mafunzo ya ufugaji , bila kuangalia viwango vya elimu uliyonayo na mazingira uliyotokea. Mafunzo yote yapo kwa nadharia na vitendo. Sehemu ya vitendo itajumuisha kutembelea sehemu yetu ya utotoleshaji na kiwanda chetu cha uzalishaji wa chakula.
- KOZI YA ULEAJI WA KUKU WA NYAMA
Ni kozi ya siku tano, hutolewa kuanzia siku ya jumatatu hadi siku ya ijumaa. Itakujenga wewe mfugaji kupata elimu ya bora kuhusu kuku wa nyama. Ili kuweza kupata uzito stahiki ndani ya muda mfupi, elimu ya FCR, masuala ya masoko , biashara na utunzaji kumbukumbu ni miongoni wa vitu utakavyojifunza
- KOZI YA UFUGAJI KUKU WA MAYAI
Ni kozi ya siku 5, hutolewa kuanzia siku ya jumatatu hadi ijumaa, itakuwezesha kupata mayai bra kutoka kwa kuku wako wa mayai, kwa kuzingatia ratiba ya mwanga, ratiba ya ulishaji chakula na kuzingatia mbinu bora za udhibiti wa vimelea. Na pia itakuwezesha kutambua dalili za mwanzo zitakazo kuambia kwamba kuku wako ni wagonjwa. Elimu ya biashara, masoko na utunzaji kumbukumbu ni miongoni mwa vitu vitakavyoundishwa.
- KOZI YA UFUGAJI KUKU KWA UJUMLA
Kozi ya ufugaji kuku kwa ujumla inahusisha elimu ya kuku wa nyama na kuku wa mayai. Kozi hii inakupatia uhuru wewe mfugaji iwapo hujui ni wapi unapeleka wapi biashara yako. Ni kozi ya siku sita na hutolewa kutoka siku ya jumatatu hadi jumamosi
- KOZI YA ULEAJI WA VIFARANGA
Kozi hii ni miongoni mwa mradi wa APMI, lakni kila mmoja anakaribishwa kujiunga. Kama wewe ni mfugaji na unahitaji kuuza kuku wako wa siku 28, kozi hii itakufaa. Hutolewa kwa siku tano kuanzia jumatatu hadi ijumaa. Utajifunza mbinu bora za uleaji vifaranga. Masomo kuhusu joto, mzunguko wa hewa, chanjo na afya ya kuku hufundishwa na mengi zaidi.
- KOZI YA USHAURI WA KIUFUNDI
Kozi hii hutolewa kwa siku saba, kuanzia jumatatu hadi jumapil. Kozi hii huusisha elimu ya ulinzi dhidi ya vimelea,usiamamizi wa shamba,usimamizi wa mazingira na utatuzi wa shida. Kozi hii huusisha elimu ya utatuzi wa shida anazokutana nazo mkulima. Mfugaji pia atajifunza jinsi ya kumpasua kuku na kuona mabadiliko ya ndani. Bila kusahau elimu ya uongozi na mawasiliano shambani. pia kinachohitajika katika kozi hii ni kukamilisha kati ya kuku wa Nyama ,Mayai au ufugaji wa kuku kiujumla.
KWANINI MFUGAJI AJE KWENYE KITUO CHA MAFUNZO CHA SILVERLANDS (T-PEC)
- KUONGEZA NA KUPANUA UJUZI JUU YA UFUGAJI BORA WA KUKU
Silverlands ni shirika kubwa lililojikita katika uwekezaji kwenye nyanja ya Ufugaji wa kuku. Shirika lina vitengo vingi ambavyo vinatoa fursa kubwa kwa washiriki kujifunza kwa nadharia na vitendo. Hii itawafanya washiriki waweze kupata na kukuza ujuzi katika ufugaji
- kupunguza vifo kipindi cha kulea vifaranga
- aina za vyakula na viwango vya ulishaji
- kuongeza ufahamu juu ya kuku
- umuhimu wa kutunza kumbukumbu.
- KUFANYA UFUGAJI NA UZALISHAJI WENYE MAFANIKIO
Kupitia Silverlands pamoja na wataalamu waliobobea katika ufugaji wa kuku na mafunzo yanayotolewa katika kituo chetu, mshirki atapata ujuzi na uelewa mkubwa zaidi katika vitu vifuatavyo;
- Namna gani unaweza kufuga kuku wa nyama na wa mayai
- Kukuza kipato kupitia ufugaji wa kuku wenye tija
- Namna gani unaweza kutafuta masoko
- Namna gani unaweza kuzuia magonjwa.
Comments
3 comments
🐥🐥
Naomba nielezwe kituo chenu cha mafunzo kiko wapi. Nataka nilete kijana wangu ana nia ya kuanza kufuga. Niambie vile vile gharama za mafunzo
Naomba kujuwa gharama za mafunzo kwa full course.
Please sign in to leave a comment.