MKULIMA ALIEFANIKIWA KUPITIA UFUGAJI WA SASSO. Follow
Sekta ya kilimo na ufugaji nchini Tanzania inaibuka kwa kasi Zaidi hasa katika ufugaji wa kuku, kwa maana ndio ufugaji pekee wenye kipato cha haraka zaidi na ni rahisi zaidi kuuendesha.
Mahitaji ya kuku kwa maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya Tanzania bado ni makubwa kutokana na mambo mawili tofauti ikiwepo Afya na kipato.
Kutokana na uhitaji huu mkubwa wa kuku soko la ndani kwa kuku na mayai lina uwezekano wa kuendelea kukua kwa kasi Zaidi.
Ufugaji wa kuku ni moja kati ya ujasiriamali bora zaidi na wenye faida sana katika suala zima la ubadilishaji wa maisha ya mfugaji. Faida hizo utaweza kuzipata endapo tu utaweza kuzingatia na kufuata maelekezo ya ufugaji bora wa kuku. Silverlands Tanzana Limited wanazalisha vifaranga bora na chakula bora ili kumpa thamani halisi mfugaji. halikadharika wanatoa mafunzo ya ufugaji bora wenye tija kwa nadharia na vitendo ndani ya muda wa wiki moja kwa kozi. Pia wanatoa mbinu za utafutaji wa masoko.
Emily ni moja ya wafugaji ambao wamefanikiwa kupitia ufugaji wa kuku. Emily aliamua kufuga kuku aina ya sasso. Tokea ameanza ufugaji wa kuku aina ya sasso hajaona tabu yeyote kuwafuga na kuwatunza, pia kuku aina ya sasso ndio walio mfanya mpaka akaweza kuwa mkulima bora wa mwaka katika sherehe za nane mwaka huu. Sasso ni aina ya kuku ambae unaweza kumfuga bila gharama kubwa na akabadilisha kwa asilimia kubwa maisha yako. kwa maelezo zaidi pitia makala iliyopita kupitia https://silverlandstanzanialtd.zendesk.com/hc/en-us/articles/360012496218-FAHAMU-KUHUSU-KUKU-AINA-YA-SASSO-
Emily anasema" Asanteni sana na hongera Silverlands kwa kunifanikisha kufikia hapa nilipo, nilizingatia ndio maana niko hapa. Nadhani bila ninyi kunipa mafundisho nisingeweza kufanikiwa." Mama emily anazungumzia mafundisho kupitia kituo chetu cha mafunzo ambacho pia nimetoa maelekezo yake zaidi katika makala za hapo awali ila pia unaweza kupata maelekezo zaidi https://silverlandstanzanialtd.zendesk.com/hc/en-us/articles/360012393878-KITUO-CHA-MAFUNZO-CHA-SILVERLANDS-TANZANIA-LIMITED-T-PEC- ama kwa kupitia tovuti yetu ambayo itakupeleka moja kwa moja katika kurasa za kituo hicho https://www.silverlandsptc.com/
Lakini pia Emily anasema " amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ufugaji wa sasso kwani mwanzo alitumia mbinu ya kuwa anachoma kuku na kuwauza na hapo ndipo aliwavutia sana wateja wake na pia kuwahamsisha wengi zaidi kutaka kuanza kufuga kuku aina ya sasso pia."
Jina: Emily Singai.
Ni kwa namna gani unadhani silverlands tanzania imewasaidia wanawake kufikia malengo yao. ?
Emily " Kwanza kabisa binafsi hapo awali nilikua nikifuga kuku wa kienyeji lakini nikaona hawana tija kabisa kwani wanachelewa sana na hata mimi nachelewa pia. lakini baada yakufika katika kituo chenu cha mafunzo ndipo nilipoona mafanikio ya kuku aina ya sasso. kwasababu, kwanza wanakua haraka mno ukiwapa chakula bora ukiwatunza vizuri basi wana faida sana.
Kituo Cha mafunzo cha Silverlands kimechangia kwa namna gani Kwa wewe kufikia malengo yako?
Emily " kituo cha silvelands kimenisaidia sana kwa sababu mwanzo nilipoacha kufuga kuku wa kienyeji nilianza kufuga kuku wa sasso lakini bila kuhudhuria mafunzo ya silvelands, Kiukweli nilikua nikichukua vifaranga (600) mia sita basi vifaranga mia nne vitakufa. Lakini tokea nimehudhuria mafunzo ya ufugaji silverlands basi kuku wangu wakifa basi ni Saba (7) au wawili (2). kwa hivyo naweza kusema ni kwa asilimia tisini na tisa mafunzo yale yamenisaidia sana na nashukuru kwa hilo."
Unaweza kuwashauri nini wakulima kuhusu kuku wa sasso?
Emily" Ningependa niwashauri tu kwamba wasichelewe bado mapema, wafike silverlands wajifunze na waanze kufuga kuku aina ya sasso. Kuku aina ya sasso wanastahimili sana magonjwa pamoja na ni wepesi zaidi kufugika. Pia chanjo ya silverlands ni bora sana kwa kuku. hivyo ningependa kuwashauri wasifuge kiholela wafuge kibiashara na kwa malengo zaidi."
Idadi kubwa ya wateja wangu pia nawafundisha kuhusiana na sasso na namna bora ya kuwalea na kufuga kibishara zaidi. Pia hata kwenye nane nane nilijaribu kuwafundisha wateja wangu na kuwapa maelekezo zaidi kuhusuiana na kituo chenu cha silverlands.
Unawashauri nin wafugaji ambao bado hawajafika kujifunza katika kituo chetu cha mafunzo?
Emily" Kiukweli nawashauri wakulima wengi sana ili kuja kujifunza katika kituo chenu cha mafunzo, na mpaka sasa waliofika kujifunza huko ni wengi mfano mwezi uliopita nilwaleta wafugaji wanne kutoka Mbeya, Dar es saalam, pamoja na hapa chalinze. na bado naendelea kuwashauri wafike hapo silverlands ili kujifunza zaidi.
Huyo ni Emily Singai mkazi wa chalinze ni moja kati ya wafugaji ambao wamenufaika Zaidi kupitia ufugaji wa sasso. Emily ni kitengo mama cha ufugaji kwa maana anawakuza vifaranga wa kuanzia siku moja na kuanza kuwauza wakiwa wamefika mwezi mmoja na kuendelea.
Kwahivyo basi hata wew unaweza kunufaika kupitia ufugaji wa kuku kwakua muda wako ni sasa. Fuga kwa maendeleo, Ongeza afya na kipato.
Silverlands Tanzania Limited.
Comments
0 comments
Please sign in to leave a comment.