MIKUTANO YA UHAMASISHAJI KANDA YA ZIWA. Mwezi wa Pili, 2021 Follow
Mwanzoni mwa Februari Timu ya Masoko imefanya Semina na mikutano ya uhamasishaji katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na wilaya zake lengo ni kuongeza uelewa juu ya lishe bora kwa kula nyama ya kuku Pamoja na mayai na kuongeza mapato kupitia ufugaji wa Kuku kibiashara, Pia kumsaidia mwanamke kuweza kumiliki biashara kupitia ufugaji wa kuku.
Kwa kushirikiana na mshauri wa Shirika la Kuku Duniani tumesaidia kuongeza uelewa juu ya masuala ya jinsia na lishe katika familia na jamii kwa ujumla.
Kuku ni chanzo kizuri cha protini na lishe bora, na ana faida nyingi kiafya. Sasso ni kuku wa kienyeji aliyeboreshwa, Sasso ni kuku wa nyama Pamoja na mayai, Ni Kuku anayekua haraka ikilinganishwa na kuku wa kienyeji, anataga mayai mengi hadi 240 katika wiki 72, Mwenye kustahimili magonjwa na vile vile hatumii dawa yoyote ili aweze kukua.
Pamoja na usimamizi mzuri kutoka kwa Kitengo Mama , Sasso anafikia hadi uzito kati ya gramu 700 hadi gramu 750 , Hii humsaidia Kitengo Mama kumuza sasso wa mwezi mmoja kwa Shilingi 5000/=
Katika miezi 2.5 Sasso anaweza kufikia uzito wa 2kg hadi 2.5kg na kuuzwa hadi TZS 15,000 /
Mfugaji wa kuku aliyefanikiwa lazima awe na ustadi na maarifa juu ya usimamizi bora wa Kuku, Usalama wao, Pamoja na chanjo.
Kituo chetu cha Mafunzo ya Kuku huko Makota kimekuwa msaada mkubwa kwa wafugaji wengi kufanikiwa sana juu ya ufugaji wa kuku kupitia ujuzi mzuri wa mafunzo na kozi zitolewazo hapo
Silverlands kupitia mpango wa APMI, Timu yetu ya masoko imehamasisha katika wilaya ambazo ambazo wapo kikazi. Wilaya hizi ni Magu, Kwimba, Misungwi na Sengerema huko Mwanza, Chato, Mbogwe na Nyang’hwale, huko Geita na Kwa Mkoani Shinyanga ni Kahama na Wilaya ya Shinyanga.
Uhamasishaji unasaidia kuzisikia changamoto za wafugaji na kuwapa ushauri na mbinu za ufugaji bora na wenye tija.
Comments
0 comments
Please sign in to leave a comment.