FAHAMU KUHUSU KUKU AINA YA SASSO. Follow
MPANGO WA KUKUZA UFUGAJI WA KUKU AFRIKA.
Mpango huu unawapa silverlands tanzania limited (STL) fursa ya kutekeleza mkakati utakaofungua milango kwa wafugaji wa vijijini kupata mbegu bora ya kuku. Pia STL inatoa msaada wa kitaalamu kwa wafugaji wadogowadogo.
Randall Ennis, mkurugenzi mtendaji wa Word Poutry Foundation alisema; "lengo letu ni kuzifikia kaya milioni 2.5 Tanzania na nigeria ifikapo mwishoni mwa mpango huu wa miaka minne.
SASSO
SASSO ni kuku ambao mfugaji anaweza kuwafuga kwaajili ya mayai lakini pia kwaajili ya nyama. Pia ni kuku ambao wanakua katika mazingira ya aina yeyote kutokana na namna ya ufugaji utakao amua kuwafuga. Unaweza kuwafuga ndani tu kama kuku wa nyama au mayai, pia unaweza kuwafuga kama kuku wa kienyeji kwa kuwaachia nnje (kujitafutia chakula na maji).
SASSO ni aina ya kuku ambao wana ladha ya kipekee kabisa kuliko aina yoyote ile ya kuku vilevile ni aina ya kuku wenye nguvu sana (hard breeds or tough breeds) ambao wana weza kuishi katika mazingira ya aina yeyote. Na kitu cha muhimu zaidi ni kwamba kuku hawa hawapati magonjwa kirahisi kulingaisha na kuku aina nyingine.
SASSO wana julikana kama kuku ambao wana rangirangi nyingi sana na kuku mmoja akitaga mayai yakitotolewa ni lazima vitoke vifaranga vyenye rangi nyingi yaani kila kifaranga kina kuwa na rangi yake.
Kuku huyu aina SASSO amefanyiwa majaribio kwa umakini na programu ya african chicken genetic gain(AGGG), katika nchi za tanzania nigeria na ethiopia.
Silverlands Tanzania limited (STL) imefanya majaribio na SASSO mbalimbali, na kuku aliyependwa zaidi Tanzania ni X- Rainbow(Mwenye manyoya ya rangi mchanganyiko).
KWANINI UFUGE SASSO
-
Kuongeza kipato
Kuku aina ya SASSO ni wepesi kufugika, Hawaitaji uangalizi wa hali ya juu. Vilevile aina yake ya malisho au ulishaji ni sawa na kuku wa kienyeji. Kuku hawa wana matokeo bora zaidi kuzidi kuku wa kienyeji kwakua wanakua haraka na pia kuku mmoja anauwezo wa kutaga mayai 240 kwa muda wake wote tofauti na kuku wa kienyeji ambapo kuku mmoja hutaga mayai chini ya 100 kwa muda wake wote.
SASSO huanza kutaga kuanzia kati ya wiki ya 18-20 na baada ya hapo hutaga mayai mpaka wiki 72. SASSO anakua na uzito wa kuanzia 1.2kg baada ya siku 35 hivyo kumpa nafasi kubwa mkulima ya kuanza kujiingizia kipato mapema kupitia mayai na nyama kwa pamoja.
Kuku hawa wana matokeo mara tatu zaidi ya kuku wa kienyeji, hivyo basi kama mkulima na unapenda kukuza kipato chako na kufikia ndoto zako, SASSO ni chaguo lililo bora zaidi kwa kuyafikia malengo yako na kutimiza ndoto zako.
- Kuwawezesha wanawake
Moja ya malengo ya kuwa na kuku wa SASSO ni kumuwezesha mwanamke. Tunamuwezesha mwanamke katika sehemu mbali mbali, kwakua kuku hawa wanaweza kufugwa kwa na mtu wa jinsia yeyote na mahala popote. Cha muhimu kabisa ni kwamba hawaitaji uangalizai mkubwa kama ilivyo kwa kuku wa nyama na mayai. Sasa basi SASSO ana kuwezesha mwanamke katika sehemu tatu ambazo ni;
- Heshima
Kupitia SASSO utaweza kujiingizia kipato chako mwenyewe hivyo kukupa nafasi ya wew kujitegemea mwenyew kwa kutotegemea mtu mwingine,
- Uhuru wa kipato
Kwakua kupitia kuku aina ya SASSO utakua ukijiingizia kipato chako mwenyewe hivyo itamuwezesha mwanamke kuwa na uhuru wa kipato chake mwenyewe, kwa mfano kufanya unachopenda kwa muda utakaopenda. kama ilivo sera yetu chagua sasso kuongeza kipato.
- Maamuzi
Kupitia SASSO mwanamke unaweza kua na maamuzi yako mwenyewe kwa sababu, SASSO inakupa uhuru wa kujiingingizia kipato chako , pia SASSO ana virutubisho vyote hivyo kua na afya bora ni sababu tosha ya wew kama mwanamke kuwa na maamuzi yako mwenyewe.
Faida ya kuku aina ya SASSO
Kuku wa SASSO ana uwezo wa kukidhi mahitaji yanayoendelea kukua ya kuku anaeweza kufugwa kwa matumizi mbalimbali, anaweza kuishi katika mazingira tofauti, asiehitaji uwekezaji mkubwa, mwepesi kufuga na anaehitajika katika soko la kuku wa rangi mchanganyiko, hivyo kusaidia kuongezeka kwa kipato cha mkulima wa Tanzania vijijini
CHANJO
Silverlands tanzania tunajivunia matumizi ya chanjo zenye ubora wa hali ya juu kabisa tunazotumia kuchanja vifaranga wa SASSO siku ya kwanza baada ya kutotolewa. tunatumia vifaa bora vya kisasa katika kuchanja vifaranga. ifuatayo ni programu ya chanjo ya vifaranga wa SASSO:
- Vectomune ND + respens - Ugonjwa wa Marek's na Kideli
- Vectomune FP & MG - Ndui
- Transimune IBD - Ugonjwa wa Gumboro
- Vitabron L - IB & ND
Kwa kuzingatia programu hii ya chanjo, mkulima anashauriwa pamoja na kuzingatia ushauri kutoka kwa daktari wake wa mifugo wawakilishi wetu kutoka silverlands ambao huwatembelea wakulima wote nchini Tanzania wanaojihusisha na ufugaji wa kuku kwa ujumla na kuwapa msaada wa kiufundi pamoja na kujua maendeleo yao katika swala zima la ufugaji. Chanjo ya mdondo na mkamba wa kuambukiza inatakiwa itolewe kwa kuku wenye siku 10,18 na 28 na kila baada ya wiki sita (6) mpaka watakapouzwa.
SASSO Ni Ufunguo wa Fursa “KUKU WA KIJIJINI – HAZINA ILIYOFICHIKA”
Comments
3 comments
👍
Nahitaji kupata vifaranga vya saso
Napataje vifaranga vya sasso wa mayai?
Please sign in to leave a comment.